Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 27, 2024 Local time: 03:19

UN: Utafiti wabaini watoto wanyanyaswa na kufanyiwa ukatili Jamhuri ya Afrika ya Kati


Volker Turk
Volker Turk

Utafiti uliofanywa na wataalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati unaonyesha kusambaa kwa  ghasia za kikabila na ukiukaji mkubwa wa utaratibu kote nchini humo.

Hali hiyo imewafanya watoto kunyanyaswa na kufanyiwa ukatili wakiwa katika mikono ya makundi yenye silaha, vikosi vya ulinzi na usalama, na wanamgambo binafsi na makampuni ya usalama.

“Ni nadra kuona nchi yenye rekodi ya haki za binadamu inashtua, ambayo imesahaulika katika ulimwengu,” alisema Volker Turk, kamishna wa UN kuhusu haki za binadamu katika hotuba ya ufunguzi kwenye baraza la haki za binadamu katika UN Ijumaa.

“Watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kila siku wanakabiliwa na uhalisia wa kuongezeka kwa ghasia ambako khofu ilitumika kama silaha na kuleta kiwewe sana, kutokana na miaka kadhaa ya ghasia.”

Alisema watoto hawajabakishwa kukumbwa na vita hivi ambavyo vimekuwa vikiendelea tangu mwaka 2012, akieleza kuwa wasichana hasa ndiyo wananyanyaswa kwa vitendo vibaya vya uhalifu wa ngono vinavyo husishwa na vita.

“Mwaka 2022, Kitengo cha Haki za Binadamu kimerekodi watoto 647 walikuwa waathirika wa ukiukaji wa haki za watoto.

Uhalifu mwingi ulihusu kuwatumia watoto katika vita, kushambulia heshima yao ya kimwili, uhuru wao, kuwaweka kiholela kizuizini, na ukatili wa kingono unaohusishwa na vita,” alisema.

Ripoti zilizopokelewa na ofisi ya haki za binadamu ya UN zinakadiria kuwa vikundi venye silaha vilivyosaini mkataba wa amani mwaka jana vilihusika kwa asilimia 35 na matukio ya unyanyasaji yaliyorikodiwa, ikiwemo mauaji, utekaji, kuwekwa kizuizini, kuwabughudi, uharibifu wa miundombinu na kunyang’anya mali.

Virginia Gamba, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa UN kuhusu masuala ya watoto na mizozo ya silaha alisema idadi ya ukiukaji mkubwa uliotendwa dhidi ya watoto mwaka 2022 ulipungua ukilinganisha na miaka iliyopita.

Hata hivyo aliongeza kusema kuwa vita viliendelea kuwaathiri idadi kubwa ya wavulana na wasichana huku wengi wao wakiuawa na kukatwa viungo kutokana na kupigwa risasi na mabaki ya mabomu.

Ni ripoti ya Lisa Schlein wa VOA, Geneva.

XS
SM
MD
LG