Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 01, 2024 Local time: 03:21

Wanajeshi wa Sudan Kusini wawasili DRC


Wanajeshi wa Sudan Kusini wamewasili mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumapili, mwandishi wa habari wa AFP aliwaona, wakijiunga na jeshi la kikanda katika eneo lililokumbwa na waasi wa M23.

Takriban wanajeshi 45 walionekana wakiwasili katika mji wa Goma majira ya asubuhi, huku wanajeshi wengine wakitarajiwa kuwasili katika tarehe za baadaye.

Wanajeshi hao wa Sudan Kusini ni sehemu ya jeshi la nchi saba za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambalo liliundwa mwezi Juni mwaka jana ili kuleta utulivu mashariki mwa DRC.

Sehemu kubwa ya eneo hilo inakabiliwa na makundi yenye silaha, urithi wa vita vya kikanda ambavyo vilipamba moto katika miaka ya 1990 na 2000.

Tangu kuibuka tena kutoka katika hali ya utulivu mwishoni mwa 2021, waasi wa M23 pia wameteka maeneo mengi katika jimbo la Kivu Kaskazini na kusonga mbele kilomita kadhaa kuukaribia mji mkuu wa Goma.

XS
SM
MD
LG