Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 21:02

Msumbiji inahitaji msaada kwa ajili ya wakimbizi kutoka DRC


Wakimbizi wakiwa wanasubiri msaada, Nampula, Msumbiji
Wakimbizi wakiwa wanasubiri msaada, Nampula, Msumbiji

Mwakilishi wa shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa mataifa nchini Msumbiji Samule CHakwera, amesema wakimbizi wanaokimbia vita katika nchi Jirani ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wametatiza hali ya kibindamu kuwa mbaya zaidi kaskazini mwa Msumbiji.

Afisa huyo wa umoja wa mataifa ameiambia VOA kwamba shirika la kuhudumia wakimbizi linahitaji rasilimali za ziada kuwashughulikia wakimbizi na wanaoomba wanaowasili Msumbiji, pamoja na raia wa msumbiji ambao wamekoseshwa makazi.

"Wanatokea Kivu kaskazini na kivu kusini ambako hali ya huko bado hali sio nzuri. Kwahiyo hali yao bado haijapatiwa ufumbuzi. Tuna wengine wanaoishi maisha ya kawaida katika jamii, na wengine wako mjini Maputo, Beira na Tete lakini ni wachache sana."

Mpigano makali kati ya makundi ya waasi na wanajeshi wa serikali mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, yamewasukuma maelfu ya raia wa Congo kukimbia makwao.

Mnamo mwezi Februari, karibu watu 300,000 walikimbia makwao kutoka maeneo Rutshuru na Masisi, jimbo la Kivu kaskazini.

Hivi sasa idadi ndogo ya watu hao wamevuka mpaka na kuingia kaskazini mwa Msumbiji, eneo ambalo vile vile linakabiliwa na mashambulizi kutoka kwa makundi ya waasi wa kiislamu wanaopambana na majeshi ya serikali katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Cabo Delgado.

Kulingana na umoja wa mataifa, Msumbiji ni mwenyeji wa wakimbizi 30,000, baadhi yao wanaomba hifadhi.

9,500 kati yao wanaishi katika kambi ya Maratane, katika jimbo la Nampula.

19000 wanaishi maeneo ya mijini na familia ambazo zinawapatia makazi.

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la umoja wa mataifa limesema kwamba linashirikiana na serikali ya Msumbiji kutoa msaada wa kuokoa maisha na ulinzi kwa watu ambao wamekoseswa makazi.

Chakwera amesema kwamba idadi kubwa ya wakimbizi wa muda na wale wanaoomba hifadhi kutoka DRC imepelekea Msumbiji kukabiliwa na changamoto za kutoa msaada kwao.

"Kwa hivyo, tunaomba ufadhili zaidi kutoka kwa wahisani kwa ajili ya vitu kama vile makazi tunahitaji makazi thabiti kwasababu ya hali ya hewa. Huo ndio msaada mkubwa tunaoomba kutoka kwa washirika wa kimataifa."

Sehemu za nyanda za chini za pwani ya Msumbiji, zinashuhudia maafa na uharibifu kila mara kutokana na hali mbaya ya hewa.

Umoja wa mataifa hutoa msaada wa dharura kila mara vimbunga vinapopiga sehemu hiyo kila mara.

Kimbunga Freddy kilipiga Msumbiji mara mbili mwezi Februari na Machi, na kusababisha uharibifu mkubwa, kuua darzeni ya wat una kupelekea watu 250,000 kukoseshwa makazi katika sehemu za kati na kaskazini mwa Msumbiji.

XS
SM
MD
LG