Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 23:23

Watu 19 wafariki katika maporomoko ya ardhi mashariki mwa DRC


Ramani ya DRC

Maporomoko ya ardhi yameua watu 19 Jana Jumapili mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, maafisa wa eneo hilo wamesema.

Maafa hayo yalitokea majira ya asubuhi katika kijiji cha Bulwa, wilaya ya Masisi katika jimbo la Kivu Kaskazini, kwa mujibu wa Chadrack Mbukanirwa Ndibanja, mmoja wa viongozi wa kijiji hicho.

Amesema watu 19 walifariki katika maporomoko hayo, na shughuli za kutafuta waathirika zaidi zitaendelea leo Jumatatu.

Alphonse Musheba Mihingano, kiongozi wa eneo hilo, amethibitisha kwamba miili 19 ilipatikana lakini akasisitiza kuwa idadi hiyo ya vifo ni ya awali.

Amesema Akina mama 25 na watoto wao, walikuwa wanafua nguo kwenye mto chini ya mlima wakati udongo ulipoporomoka na kuwafukia baadhi yao.

Mkazi wa kijiji cha Bulwa Musafiri Balume alitoa maelezo kama hayo, akisema alimpoteza dada yake katika maporomoko hayo ambayo yalitokea wakati wa mvua kubwa.

XS
SM
MD
LG