Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 04:13

COVID-19 : Uhispania yaruhusu baadhi ya wafanyakazi kurejea makazini


Abiria wakiwa wamevalia maski wakitumia usafiri wa umma kaika Stesheni ya treni ya Atocha, Madrid Aprili 13, 2020, makati wakati baadhi ya makampuni yakiwa tayari kuanza shughuli zao ifikapo mwisho wa amri ya serikali ya wiki mbili kusimamisha shughuli zote ambazo sio muhimu. ( J

Uhispania imeanza kulegeza baadhi ya masharti ya kutotoka nje Jumatatu kwa kuwaruhusu wafanyakazi wa sekta ya viwanda na ujenzi kurejea makazini.

Wakati bado kuna wasiwasi wa kuenea kwa virusi hivyo, makampuni yanatakiwa kuwapa wafanyakazi vifaa vya kujihami na kuhakikisha kuwa pendekezo la watu kutokaribiana kwa mita mbili linazingatiwa.

Spain ni moja ya nchi zilizoathiriwa zaidi na janga la corona ikiwa inazaidi ya maambukizi yaliyopimwa na kuthibitishwa 165,000 na vifo 17,000. Sehemu kubwa ya nchi hiyo imekuwa chini ya amri ya kutotoka majumbani kwa kipindi cha takriban mwezi mmoja.

Waziri Mkuu Pedro Sanchez amesema Jumapili janga hilo ni tishio siyo tu kwa athari za kiafya, lakini pia kiuchumi na kijamii.

Hivyo basi, kukabiliana na janga hili kunahitaji hatua mchanganyiko zinazozuia maambukizo, zinazowezesha mifumo yetu ya afya kuimarika na wakati huo huo kuzuia uchumi wetu usidumae na kuporomoka kutokana na athari mbaya zinazoweza kufanya ajira ya nchi yetu kutetereka,” Sanchez amesema.

Uwiano kati ya muda gani kuendeleza amri ya kutotoka majumbani na wakati gani kuwaruhusu warudi makazini ili kuimarisha uchumi uendelee kuzalisha ndilo hivi sasa linapimwa na serikali zote ulimwenguni.

Waziri Mkuu wa Korea Kusini Chung Sye-kyun amesema Jumatatu maafisa walikuwa wanajadili miongozo mipya inayowezekana itakayoweza kuendeleza suala la kutokaribiana baina ya watu wakati ikiruhusu “shughuli za kiuchumi na kijamii kufanyika.”

Korea Kusini imeshuhudia idadi ya maambukizi mapya ya kila siku ikiendelea kupungua, ambapo serikali imetangaza Jumatatu maambukizi 25 mapya.

Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria nia yake kuruhusu shughuli za kiuchumi kuendelea kama kawaida haraka iwezekanavyo.

Uongozi wake umeshauri watu kutotoka majumbani iwapo itawezekana hadi mwisho wa mwezi, wakati magavana wa majimbo mengi kati ya 50 wamechukua hatua zaidi na kuamrisha watu kutotoka majumbani ila tu kwa ajili ya kufanya mazoezi na kununua mahitaji yao.

Mtaalam wa ngazi ya juu wa magonjwa ya kuambukiza Dkt Anthony Fauci amesema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CNN Jumapili kuwa anafikiri baadhi ya amri zilizowekwa pengine zinaweza kuondolewa mapema mwezi ujao.

“Ni matarajio yetu kuwa ifikapo mwisho wa mwezi tunaweza kutathmini hali hii na kusema, sawa, kuna kitu chochote hivi sasa tunaweza kuruhusu kifanyike katika hali ya usalama na tahadhari? Iwapo ndio, tufanye. Ikiwa hapana, basi tuendelee kuzuia,” Fauci amesema.

Ameongeza kuwa suala la msingi litakuwa uwezo wa kutambua mtu yeyote ambaye atapata maambukizi, kuwatenga watu hao, na kufuatilia nani walikuwa wamekaribiana naye, na kwamba juhudi zozote za kurejesha nchi katika hali ya kawaida itategemea hali halisi ilivyo katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Mapema Jumatatu, kulikuwa na watu milioni 1.85 walithibitishwa kuwa na maambukizi duniani kote, vifo 114,000, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. Kati ya idadi hiyo Marekani inamaambukizi 550,000.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG