Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Agosti 03, 2021 Local time: 16:16

Saudi Arabia yasitisha mapigano kutoa fursa kufika misaada ya dharura kukabiliana na corona Yemen


Madaktari wakiwa katika moja ya wodi kuhudumia wagonjwa huku wakijikinga na virusi vya corona kwa kuvaa maski mjini Sanaa, Yemen Machi 17, 2020. Picture taken March 17, 2020. REUTERS/Khaled Abdullah

Umoja wa majeshi yanayo ongozwa na Saudi Arabia ambayo yamekuwa yakipigana na waasi wa Yemen, Wahouthi kwa miaka mitano yametangaza kusitisha mapigano kwa wiki mbili kuanzia Alhamisi kufuatia wito wa Umoja wa Mataifa wa kuwepo amani wakati huu ambapo dunia inakabiliana na janga la virusi vya corona.

Baada ya kutoa wito huo mwezi Machi, Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres aliripoti wiki iliyopita kuwa pande zote hasimu katika nchi mbalimbali zimekubali wito huo, ikiwemo Cameroon, Libya, Sudan Kusini, Syria na Ukraine.

Duniani kote kufikia Alhamisi watu waliopimwa na kuthibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona takriban milioni 1.5 na vifo 89,000. Wale waliopona ni kufikia leo ni 337,276.

Juhudi za UN zimejikita sio tu katika kusitisha vita hivyo, lakini kutoa nafasi kwa makundi ya misaada ya kibinadamu na serikali mbalimbali kupata fursa bora zaidi ya kufikisha misaada inayohitajika haraka na kujaribu kuzuia kuenea kwa virusi vya corona katika jamii ambazo zina mazingira hatarishi zaidi duniani.

Kamati ya Kimataifa ya Ukoaji imetoa ripoti mpya Alhamisi ikitaka masuala ya misaada ya dharura yazingatiwe.

Imeainisha vifaa vya tiba muhimu ambavyo vinaupungufu katika nchi zilizokuwa na maambukizi zaidi kama vile Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya, wakati “nchi nyingi zilizoathirika na vita na kusambaratishwa hawana chochote cha kuanzia kukabiliana na maradhi hayo."

Ripoti hiyo inasema nusu ya mahospitali tu nchini Yemen zinatoa huduma kikamilifu, lakini thuluthi mbili ya wananchi wa nchi hiyo hawana huduma ya afya. Pia imeeleza juu ya uhaba wa vitanda na vifaa vya kusaidia kupumua katika vyumba vya watu mahtuti huko Sudan Kusini, Syria Kaskazini na Venezuela.

Nchi nyingi zimeanzisha amri ya kutotoka majumbani kuzuia watu kwenda shuleni, makazini, au kuenda kununua bidhaa ambazo sio muhimu, kwa matarajio ya kuzuia maambukizi mapya.

Japan imepitisha amri ya hali ya dharura katika mji wa Tokyo na maeneo mengine mapema wiki hii, na Alhamisi wizara yake ya afya imeripoti maambukizi mapya yaliyopimwa 500.

Baadhi ya viongozi wamesema wanaimani kuwa nchi zao zimeshuhudia mpito wa hali mbaya kuliko zote za janga hilo na wanatarajia kuanza kuruhusu baadhi ya shughuli za kila siku kuendelea kama kawaida.

Jamhuri ya Czech Alhamisi imeruhusu kufunguliwa tena mahitaji ya kawaida na maduka ya vifaa vya ujenzi. Nchi hiyo imeripoti maambukizi 5,000 na Waziri wa Afya Adam Vojtech amesema Jumatano takwimu zinaonyesha “hadi sasa nchi hiyo iliweza kujikinga na hali mbaya zaidi ya maambukizi.”

Marekani inaongoza hadi sasa ikiwa na maambukizi 430,000. Idadi kubwa ya maambukizi hayo iko katika mji wa New York, ambako Gavana Andrew Coumo Jumatano alipongeza juhudi zilizochukuliwa za amri ya kutotoka majumbani zikionyesha kuleta tija huku akiwahimiza watu, “ Hatuwezi kusitisha hili sasa.”

Zaidi ya watu 6,000 wamekufa huko New York kutokana na virusi vya corona. Jimbo hilo limeripoti kuongezeka kwa vifo 779 Jumatano.

Hata hivyo Cuomo wiki hii ameeleza kupungua kwa wagonjwa wapya hospitalini ikiwa ni alama ya hali katika jimbo lake inaweza kuimarika muda siyo mrefu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG