Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 22:16

COVID-19 : Yemen yathibitisha maambukizi ya mtu wa kwanza


Hali ilivyokuwa mini Hadharalmout baada ya kutangazwa hali ya kutotoka nje ikiwa hatua ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona Yemen April 10, 2020. Picha na REUTERS/Ibrahim al-Bakri.

Yemen imethibitisha Ijumaa kuwepo ambukizi la kwanza la virusi vya corona lililotokea katika jimbo la kusini la Hadharalmauti lenye utajiri wa mafuta.

Kamati ya kitaifa ya dharura kwa ajili ya COVID 19 imetoa taarifa hiyo kwenye twitter bila ya kutoa maelezo zaidi. Imesema mgonjwa anaendelea vizuri na anapewa huduma za afya zinazohitajika.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameelezea wasiwasi wao wakisema iwapo virusi hivyo vitasambaa nchini Yemen, athari yake itakuwa janga kubwa, kwa sababu mfumo wa huduma za afya kwa nusu ya raia wote wa Yemen ni duni sana.

UN imeeleza kuwa taifa hilo linakabiliwa na uhaba wa vifaa muhimu vya matibabu, wataalam wa kutosha na uhaba wa vituo vya kutoa huduma.

Habari hiyo imefuatia taarifa ya sitisho la mapigano nchini kote kufuati wito wa UN ukizitaka pande zote hasimu duniani kusitisha mapigano ili kutoa fursa kwa misaada ya dharura kufikia nchi hizo kukabiliana na mlipuko wa corona.

Serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia illitangaza kusitisha operesheni za kijeshi katika kipindi cha wiki maili, lakini waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran walikuwa hawakubaliana na pendekezo hilo la serikali.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG