Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 08:49

Uganda yakamata mashoga


Washiriki wa gwaride la mashoga huko Entebbe Uganda, tarehe 8, Agosti 2015. PICHA NA AFP/ ISAAC KASAMANI.
Washiriki wa gwaride la mashoga huko Entebbe Uganda, tarehe 8, Agosti 2015. PICHA NA AFP/ ISAAC KASAMANI.

Polisi wa Uganda walisema Ijumaa wamewakamata wanaume sita kwa "kufanya ushoga", tangazo hilo limetolewa siku moja baada ya Rais Yoweri Museveni kuwaelezea mashoga kama watu "waliopotoka".

"Kupitia mtandao wa kijasusi, tumewakamata wanaume sita katika chumba kimoja huko Jinja ambako walikuwa wakifanya ushoga," msemaji wa polisi James Mubi alisema.

"Tuliaarifiwa kuwa wanaume hao sita walikuwa ni sehemu ya kundi kubwa mjini Jinja linalojihusisha na vitendo vya ushoga na tunatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa polisi zitakazo wezesha kukamatwa kwa wanachama waliosalia wa kundi hilo."

Mji wa Jinja uko kilomita 80 mashariki mwa mji mkuu Kampala. Uganda inajulikana kwa sheria zisizostahmili ushoga – ni uhalifu chini ya sheria za enzi ya utawala wa kikoloni -- na kwa maadili makali ya Kikristo kuhusiana na masuala ya ngono kwa ujumla.

Siku ya Alhamisi, rais Museveni aliwahutubia wabunge ambao wanajiandaa kujadili sheria dhidi ya ushoga, Museveni alisema ushoga "ni mwenendo wa tabia unaokiuka maadili".

Chini ya sheria iliyopendekezwa, mtu yeyote anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja au anayejitambulisha kama LGBTQ anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 jela.

Mswaada huo unatarajiwa kujadiliwa wiki ijayo, na kura inaweza kupigwa siku ya Jumanne asubuhi.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG