Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 17:59

"Ushoga" wasababisha mwenye nyumba kumfukuza mpangaji


Raia wa Uganda wakishiriki katika Gwaride la sherehe za Kujivunia usagaji, ushoga (LGBT) katika jiji la Entebbe, Uganda. Picha na shirika la habari la AP/Rebecca Vassie.
Raia wa Uganda wakishiriki katika Gwaride la sherehe za Kujivunia usagaji, ushoga (LGBT) katika jiji la Entebbe, Uganda. Picha na shirika la habari la AP/Rebecca Vassie.

Siku chache baada ya bunge la Uganda kuamuru uchunguzi ufanyike kuhusiana na madai ya kuhamasisha kwa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja mashuleni mwezi uliopita, video ilionekana kwenye mtandao ikimtambulisha mkazi mmoja wa Kampala Eric Ndawula kuwa shoga.

Ndawula mwenye umri wa miaka 26, alisema mwenye nyumba wake alimuonyesha video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao na mtu asiyejulikana, na kisha kumpa notisi ya kumfukuza kwenye nyumba akisema kuwa nyumba yake haipangishwi kwa mtu ambaye ni shoga.

“Mimi sasa nimekuwa tishio kwa watoto wanaonizunguka kwa sababu wataniiga na kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja,” kwa utani Ndawula aliliambia shirika la habari la Reuters.

Anayoyapitia Ndawula ni moja ya matukio ya wimbi la ubaguzi na unyanyasaji dhidi ya wasagaji, mashoga , watu wa jinsia mbili na wale waliobadili jinsia. Ubaguzi ulioanza tangu bunge lilipotangaza uchunguzi wake, wanaharakati wanasema.

Zogo limezidi kuathiri jamii ya LGBT ambayo tayari iko hatarini nchini Uganda, ambako watu wenye mahusiano ya jinsia moja hupewa adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Waziri wa habari Chris Baryomunsi hakujibu maswali kuhusu athari za uchunguzi huo. Cuthbert Abigaba, mbunge anayeongoza uchunguzi huo, aliiambia Reuters kuwa "hasumbuliwi na chochote kinachosemwa na watu wa wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Chanzo cha habari ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG