Kupatikana kwa miili hiyo kumetokea kiasi cha saa 24 baada ya mlipuko huo ulioliangusha jengo la ghorofa nne katika mji wa bandari ya Mediterranean.
Wafanyakazi wa dharura wameendelea na operesheni ya uokoaji hadi Jumapili usiku kufikia majira ya alfajiri Jumatatu wakisaidiwa na kreni na taa, lakini moto uliokuwa unaendelea kuwaka chini ya kifusi ulizuia shughuli zao, na na kuifanya iwe vigumu kwa wafanyakazi wa zima moto kupeleka mbwa maalum wa kutafuta watu waliofunikwa na kifusi.
“Kutokana na matatizo maalum ya kuendesha uokoaji, kuitoa (miili kutoka eneo hilo) muda,” idara ya zimamoto ilisema katika taarifa fupi ikitangaza miili iliyopatikana.
Mamlaka za mahakama baadaye zitaendelea na zoezi la kuwatambua” waliofariki, imeongeza.
Mapema Jumapili, kabla ya kugundua miili hiyo, mwendesha mashtaka wa eneo Dominique Laurens aliwaambia waandishi wa habari kuwa watu wanane “ hawakuwa wanajibu simu walizopigiwa”.
Watu watano kutoka majengo jirani walipata majeraha madogo katika mlipuko na kuporomoka jengo, uliotokea kiasi cha saa sita na dakika arobaini usiku wa manane Jumapili (2240 GMT Jumamosi).
“Usiku wa leo, maumivu na majonzi ni makubwa,” alisema meya wa Marseille Benoit Payan katika taarifa yake.
“Huduma zote za jiji hilo, na pia jimbo hilo, linbado zinaendelea hivi sasa kwa azma ya kuwatafuta waathirika,” aliongeza.
Sababu ya mlipuko huo bado haijajulikana, lakini wachunguzi wanatafuta kujua kama inawezekana ni matokeo ya gesi iliyokuwa ikivuja.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP