Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 01:26

Burkina Faso: Utawala wa kijeshi wafunga matangazo ya kituo cha televisheni cha Ufaransa France 24


Nembo ya kituo cha televisheni cha Ufaransa, France 24
Nembo ya kituo cha televisheni cha Ufaransa, France 24

Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso Jumatatu ulisitisha matangazo yote ya kituo cha televisheni cha Ufaransa France 24 katika nchi hiyo ya Afrika magharibi baada ya kituo hicho kufanya mahojiano na kiongozi wa kundi la Al-Qaeda Afrika Kaskazini.

Burkina Faso, ambayo ilishuhudia mapinduzi mawili ya kijeshi mwaka jana, inapambana na uasi wa wanamgambo wa Kiislamu ambao ulisambaa kutoka nchi jirani ya Mali mwaka 2015.

“Kwa kumpa nafasi kiongozi wa AQIM, France 24 haikufanya tu kitendo cha kuwa idara ya mawasiliano kwa magaidi hao lakini imehalalisha pia vitendo vya kigaidi na matamshi ya chuki,” msemaji wa utawala wa kijeshi amesema, akigusia mahojiano ya tarehe 6 Machi na kiongozi wa kundi la Al-Qaeda Afrika kaskazini au AQIM, Abu Ubaydah Yusuf al-Annabi.

“Kwa hiyo, serikali imeamua kusitisha mara moja matangazo ya vipindi vya France 24 nchini kote, msemaji Jean Emmanuel Ouedraogo alisema.

XS
SM
MD
LG