Jengo la makazi huko Marseille nchini Ufaransa lilianguka Jumapili. Wafanyakazi wa huduma za dharura wanawatafuta waathirika. Takriban watu sita walijeruhiwa.
Maafisa huko Marseille wanasema mlipuko ulisikika lakini haijabainika mara moja ikiwa mlipuko ulisababisha jengo hilo kuanguka au kuanguka kwa jengo ndio kulisababisha mlipuko. Hata hivyo moto uliwaka katika eneo hilo baada ya jengo kuanguka.
Tunajaribu kuzima moto wakati pia tukijaribu kuokoa maisha ya waathirika walio chini ya kifusi, Lionel Mathieu, kamanda wa kikosi cha zima moto cha Marseille alisema. Majengo mawili karibu na eneo la tukio pia yameporomoka kwa kiasi fulani.