Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 03:42

Macron anamshawishi Jinping kusaidia kumaliza vita vya Russia nchini Ukraine


Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron (L) na Rais wa China Xi Jinping
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron (L) na Rais wa China Xi Jinping

Macron katika ziara yake huko Beijing alimwambia Jinping kwamba "najua ninaweza kukutegemea wewe kuirejesha Russia kuliangalia hili na kila mtu kurudi kwenye meza ya mazungumzo"

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemshawishi Rais wa China Xi Jinping kutumia uhusiano wa China na Russia kusaidia kumaliza vita vya Russia nchini Ukraine.

Macron alimwambia Xi wakati walipokutana leo Alhamisi mjini Beijing kwamba uvamizi wa Russia nchini Ukraine umeathiri utulivu wa kimataifa. Najua ninaweza kukutegemea wewe kuirejesha Russia kuliangalia hili na kila mtu kurudi kwenye meza ya mazungumzo Macron alisema.

China imependekeza mpango wa amani wa sehemu nyingi kwa Ukraine unaojumuisha wito wa kuzingatia uhuru na uadilifu wa eneo la nchi zote, lakini haitoi wito kwa Russia kuondoa vikosi vyake kutoka Ukraine.

Maafisa wa Ukraine wamesema watashiriki tu katika mazungumzo ya amani iwapo Russia itaondoa jeshi lake lote, huku Russia ikisisitiza kuwa Ukraine inatambua maeneo ambayo Russia imedai kuyanyakua.

XS
SM
MD
LG