Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 18:11

Sudan Kusini yaandaa mswaada wa katiba kuimarisha umoja wa kitaifa


Rais Salva Kiir, kulia na Makamu wake Riek Machar, wakipongezana baada ya kuapishwa kuchukua madaraka mjini Juba, Sudan Kusini, Feb. 22, 2020.
Rais Salva Kiir, kulia na Makamu wake Riek Machar, wakipongezana baada ya kuapishwa kuchukua madaraka mjini Juba, Sudan Kusini, Feb. 22, 2020.

Sudan Kusini imeanza kutayarisha mswaada wa katiba kwa lengo la kutekeleza makubaliano ya amani yanayo yumbayumba kwa karibu miaka 10 baada ya taifa hilo kujinyakulia uhuru.

Rais Salva Kiir aliongoza sherehe za kuzinduliwa utaratibu ambao ni sehemu ya makubaliano ya amani yaliyofikiwa pamoja na mpinzani wake Rick Machar mwa 2018.

Taifa hilo changa kabisa duniani limekuwa likiongozwa na katiba za mpito wakati wa miaka ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokea baada ya uhuru hapo julai 2011.

Sudan ya Kusini ilitumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe Disemba 2013 baada ya Kiir kumtuhumu Machar kupanga njama ya kumpindua.

Ugomvi huo ambao ulioshuhudia ubakaji ukitumiwa kama silaha ya vita ulisababisha vifo vya zaidi ya watu 380,000 na kuwakosesha makazi watu wengine milioni 4.

XS
SM
MD
LG