Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 03, 2022 Local time: 22:57

Riek Machar aondolewa vikwazo vya usafiri na IGAD


Makam wa rais wa Sudan Riek Machar (kushoto) akiwa na rais Salva Kiir (Kulia) Feb. 22, 2020.

Mamlaka ya ushirikiano wa serikali za nchi za pembe mwa Afrika kwa ajili ya maendeleo IGAD, imeondoa marufuku ya usafiri aliyokuwa amewekewa makam wa rais wa kwanza wa Sudan kusini Riek Machar.

Hatua hiyo inamruhusu Machar kusafiri katika nchi yoyote mwanachama wa Igad.

Machar aliwekewa marufuku hiyo wakati wa vita vya Sudan kusini.

Uamuzi huo umetolewa baada ya kikao cha viongozi wa nchi za IGAD, uliofanyika Djibouti, Jumapili.

Mkutano huo uliitishwa kujadili usalama katika kanda hiyo, Pamoja na janga la virusi vya Corona.

Zaidi ya watu 290,000 wameambukizwa virusi vya Corona na 5,400 kufariki katika nchi za IGAD.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG