Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:11

Serikali ya mseto ya Sudan Kusini kuanzisha mahakama ya mseto ya AU


Katika taarifa iliyotolewa Jumapili, Mahamat alisema uamuzi huo unakomesha ucheleweshwaji wa kuanzisha mahakama, haki ya mpito, uwajibikaji, maridhiano na taasisi za kuponya ili kuleta haki na uponyaji kwa wa-Sudan Kusini wote

Mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, anasema anakaribisha uamuzi wa serikali ya mpito ya umoja wa Kitaifa ya Sudan Kusini wa kuanzisha mahakama ya mseto ya AU kwa nchi hiyo Kama ilivyotakiwa kwenye makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwaka 2018.

Huku kukiwa na ripoti za ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu baada ya mzozo kuzuka mwaka 2013 nchini Sudan Kusini, Umoja wa Afrika uliamuru kuundwa kwa tume ya uchunguzi iliyoongozwa na Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo. Ripoti ya mwisho ya tume hiyo iliwasilishwa Oktoba mwaka 2015.

Katika taarifa iliyotolewa Jumapili, Mahamat alisema uamuzi huo unakomesha ucheleweshwaji wa kuanzisha mahakama, haki ya mpito, uwajibikaji, maridhiano na taasisi za kuponya ili kuleta haki na uponyaji kwa wa-Sudan Kusini wote. Wakati huo huo, Nyagoah Tut Put, mtafiti wa haki za binadamu kwa Sudan Kusini anasema hatua iliyofanywa na serikali ya Sudan Kusini inapaswa kutazamwa kwa tahadhari.

XS
SM
MD
LG