Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:46

Kenya kupokea chanjo ya COVID-19 kutoka Sudan Kusini


Chanjo ya AstraZeneca
Chanjo ya AstraZeneca

Kenya itapokea karibu dozi 72,000 za chanjo ya covid 19 wiki hii kutoka mpango wa Covax.

Dawa hizo zitawasili kutokea Sudan Kusini baada ya maafisa wa wizara ya afya wa nchi hiyo kusema kwamba hawataweza kuzitumia kabla ya muda wake kumalizika.

Sudan Kusini ilipokea dozi 132,000 za Astra Zeneca chini ya mpango wa Covax, mwishoni mwa mwezi Machi.

Lakini naibu Waziri wa Afya Mayen Machout amewaambia waandishi habari Jumatano kwamba hawakuweza kutumia dozi zote.

Pia serikali imetoa sababu ya bunge kuchelewa kuidhinisha matumizi ya chanjo hiyo.

Hivyo serikali ya Juba itabaki na dozi 52,000 kwa matumaini ya kuzitumia kabla ya muda wake wa Julai 18 kupita.

XS
SM
MD
LG