Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 20, 2025 Local time: 13:44

Wapiganaji wa SPLA-IO Sudan kusini waomba msamaha


Wapiganaji wa SPLA-IO
Wapiganaji wa SPLA-IO

Kundi kuu la upinzani nchini Sudan kusini - Sudan People's Liberation Army SPLA-IO, limoemba msamaha kufuatia ripoti kwamba wapiganaji wake waliwakamata wafanyakazi wa umoja wa mataifa mwezi uliopita.

Kundi hilo lilisaini makubaliani ya amani ya mwaka 2018, yaliyomaliza vita vya miaka sita na kupelekea Riek Machar kuteuliwa kama makam wa rais.

Wafuatiliaji wa utekelezaji wa mkataba huo waliripoti jumanne kwamba wapiganaji wa SPLA-IO, walikamata mfanyakazi wa umoja wa mataifa na raia kadhaa katika Kijiji cha Farajalla, jimbo la Bahr El-Ghazal, magharibi mwa Sudan kusini.

Mwakilishi wa SPLA-IO Maj Gen Martin Abucha, amekashifu tukio hilo na kuomba msamaha kwa niaba ya kundi hilo akisema kwamba waliokamatwa waliachiliwa huru.

Maj Gen Abucha amesema kwamba tukio hilo linasikitisha na kwamba hatua zimechukuliwa kuhakikisha kwamba halitatokea tena.

Wafuatiliaji wa mkataba wa kusitisha vita nchini Sudan kusini, pia wamesema kwamba wahusika wameendelea kuvunja mkataba huo na kuwalaumu kwa kukataa kuuheshimu.

Kulingana na mkataba huo, viongozi wa Sudan kusini wanatarajiwa kuunda jeshi moja la kitaifa lenye jumla ya wanajeshi 83,000.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG