Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 14:47

Shirika la ndege la Kenya kulipa mafao ya wafanyakazi


Ndege za Shirila la Kenya Airways zikiwa zimeegeshwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wakati wa mgomo
wa marubani Apr. 28, 2016. Picha na maktaba.
Ndege za Shirila la Kenya Airways zikiwa zimeegeshwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wakati wa mgomo wa marubani Apr. 28, 2016. Picha na maktaba.

Shirika la ndege la Kenya litaanzisha upya kuwasilisha michango ya kila mwezi ya wafanyakazi wake kwa mfuko wa pensheni ambayo ilisimamishwa kutokana na janga la COVID

Barua ya ndani ya shirika hilo ilionyesha Alhamisi kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, ikidai shirika hilo kusuluhisha malalamiko makubwa yaliyosababisha mgomo wa marubani.

Mwezi Novemba mwaka jana, maelfu ya abiria walikwama kufuatia mgomo wa marubani 400 walilitaka shirika hilo lianze kuchangia mafao yao na kutatua tatizo la malipo yaliyo kuwa yameahirishwa. Mgomo huo ulimalizika baada ya amri ya mahakama.

Shirika hilo, ni moja ya makampuni makubwa barani Afrika, limesema katika taarifa yake kuwa halina budi kulipa malimbikizo yote tangu mpango huo ulipositishwa mwezi Machi 2020.

Hatua hiyo inafuatia tathimini ya shirika hilo la ndege likisema “utekelezaji wa uboreshaji unaoendelea” taarifa ambayo imetiwa saini na mkuu wa idara ya wafanyakazi. Hakuna majibu yalitolewa kwa haraka na utawala la shirika hilo la ndege kuhusu taarifa hio.

Serikali inaliona shirika la ndege la Kenya kuwa muhimu kwa shuguli za utalii na kiuchumi kwa ujumla kutokana na jukumu lake la usafiri, lakini kwa miaka ya hivi karibuni limekuwa likipata hasara ambayo imelisukuma kushindwa kumudu matengenezo ya kiufundi

XS
SM
MD
LG