Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 20:04
VOA Direct Packages

Meta yakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya Kenya kuwa inaweza kushitakiwa ndani ya nchi


Meta, kampuni inayomiliki Facebook.
Meta, kampuni inayomiliki Facebook.

Meta, Kampuni inayomiliki  Facebook imekata rufaa nchini Kenya,  kupinga uamuzi  uliosema kwamba  inaweza kushtakiwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki  licha ya kutokuwa na uwepo rasmi nchini humo.

Mapema mwezi huu, mahakama ya kazi ya Kenya ilitoa uamuzi kuwa Meta inaweza kushtakiwa nchini humo baada ya aliyekuwa msimamizi wa maudhui kufungua mashtaka akidai wafanyakazi walifanyishwa kazi katika mazingira magumu.

Kwenye rufaa hiyo ambayo shirika la habari la Reuters liliweza kuiona Jumanne, kampuni hiyo ya Marekani ilihoji uamuzi wa mahakama kwamba mahakama za Kenya zina mamlaka ya kisheria juu ya kampuni hiyo ya Meta.

Meta iliajiri wafanyakazi kutoka nje kudhibiti maudhui yake kupitia Sama, kampuni yenye makao makuu Marekani na kuendesha shughuli zake nchini Kenya. Mwezi uliopita Sama ilisema haitatoa tena huduma za udhibiti wa maudhui kwenye kampuni ya Meta.

Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa msimamizi wa maudhui Daniel Motaung kwa niaba ya kundi la waliokuwa wafanyakazi wa Sama.

XS
SM
MD
LG