Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 03:23

RWANDA: Mahakama ya rufaa yaidhinisha hukumu dhidi ya Rusesabagina


PICHA YA MAKTABA - Paul Rusesabagina, akiwa mahakamani mjini Kigali, Rwanda, Feb. 17, 2021. PICHA: Reuters
PICHA YA MAKTABA - Paul Rusesabagina, akiwa mahakamani mjini Kigali, Rwanda, Feb. 17, 2021. PICHA: Reuters

Mahakama ya rufaa ya Rwanda imeidhinisha hukumu ya miaka 25 aliyopewa Paul Rusesabagina, anayezuiliwa gerezani kwa madai ya kufanya ugaidi.

Mahakama hiyo hata hivyo imekataa rufaa iliyoasilishwa na upande wa mashtaka kutaka Rusesabagina ahukumiwe maisha gerezani.

Mkosoaji huyo mkubwa wa rais Paul Kagame, na ambaye amekuwa kizuizini kwa mda wa siku 600 sasa, alihukumiwa mwaka uliopita baada ya kumalizika kwa kesi ambayo familia na wafuasi wake walitaja kama iliyojaa makosa mengi.

Mahakama ya rufaa imesema kwamba Rusesabagina amepatikana na makosa kwa mara ya kwanza na hakuna sababu ya kuongeza hukumu dhidi yake.

Mahakama hiyo vile vile imesikiliza rufaa dhidi ya hukumu waliyopewa watu wengine 20 walioshitakiwa pamoja na Rusesabagina, na ambao walihukumiwa miaka 20 gerezani.

Wanashutumiwa kwa kuunga mkono kundi la waasi lililoshutumiwa kwa kutekeleza mashambulizi mabaya yaliyosababisha vifo nchini Rwanda kati ya mwaka 2018 na 2019.

Rusesabagina ametambuliwa kwa sifa tele, kutokana na hatua yake ya kuwanusuru zaidi ya watu 1,200 wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 1994 vilivyopelekea mauaji ya watu 800,000 wengi wao wakiwa Watutsi.

XS
SM
MD
LG