Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 07:50

Mkosowaji mkuu wa serikali ya Rwanda akata kufika mahakamani


 Paul Rusesabagina, akiwa ndani ya mahakama mjini Kigali, Februari 17 mwaka wa 2021. Picha ya Reuters
Paul Rusesabagina, akiwa ndani ya mahakama mjini Kigali, Februari 17 mwaka wa 2021. Picha ya Reuters

Mkosowaji mkuu wa serikali ya Rwanda Paul Rusesabagina amekata kufika mahakamani mjini Kigali leo Jumatatu, wakati waendesha mashtaka wakijaribu kuongeza hukumu aliyopewa kuhusu mashtaka ya ugaidi kutoka miaka 25 jela hadi kifungo cha maisha.

Jaji ameahirisha kesi hadi Jumanne baada ya Rusesabagina, ambaye vitendo vyake wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 vilimsababisha kushiriki kwenye filamu maarufu “ Hotel Rwanda” huko Hollywood, kukata kuhudhuria kesi hiyo.

Rusesabagina mwenye umri wa miaka 67, na washtakiwa wenzake 20 walitiwa hatiani na kuhukumiwa mwezi Septemba mwaka jana, kwa kuunga mkono kundi la waasi wenye silaha katika kesi ambayo makundi ya kutetea haki za binadamu na wafuasi wake, walidai kuwa shutma hizo ni uongo.

Lakini waendesha mashtaka walitaka ahukumiwe kifungo cha maisha jela na kukata rufaa, wakiona kuwa adhabu hiyo ni ndogo kwa meneja huyo wa zamani wa hoteli, ambaye alitumiya wasifu wake wa kimataifa kumkosoa rais wa Rwanda Paul Kagame.

Washtakiwa wenzake wote walifika mahakamani Jumatatu.

Mmoja wa mawakili wao, Jean Rugeyo, alidai kuwa taratibu hazikufuatwa kwa namna inavyostahiki na hivyo kesi hiyo iahirishwe kwa ajili ya washtakiwa wote.

“Ndio maana tumeomba kusikilizwa kwa kesi ya leo ya rufaa kusitishwe hadi pale Paul Rusesabagina atakapojulishwa rasmi kwa kufuata sheria”, amesema.

Lakini mwendesha mashtaka wa serikali, Bonaventure Ruberwa alidai kuwa Rusesabagina, ambaye amekuwa akizuiliwa jela tangu kukamatwa kwake Agosti 2020, alikuwa amearifiwa kulingana na sheria kufika mahakamani.

XS
SM
MD
LG