Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 08:18

Waendesha mashtaka Rwanda waomba mkosoaji wa Kagame afungwe maisha


Rais Paul Kagame
Rais Paul Kagame

Waendesha mashtaka nchini Rwanda Alhamisi wameiomba mahakama ya juu nchini humo kumhukumu kifungo cha maisha jela mkosoaji mkuu wa serikali ya Rwanda, Paul Rusesabagina, kwa tuhuma za ugaidi.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Kigali ambaye amefuatilia kesi hiyo anasema waendesha mashtaka wanamshtumu Rusesabagina kwa makosa tisa, ikiwemo kuunda na kufadhili kundi haramu ambalo liliendesha mashambulizi ya kigaidi nchini humo kati ya mwaka 2018/19 na kusababisha vifo vya darzeni ya watu.

Rusesabagina hakuwepo mahakamani wakati wa kusikilizwa kesi dhidi yake na watuhumiwa wenzake 21.

Amekuwa akisusia kufika mahakamani akidai kwamba mahakama za Rwanda hazina mamlaka ya kumfuatilia kwa sababu ya uraia wake wa Ubelgiji, na kueleza kuwa mfumo wa sheria wa nchi hiyo hauwezi kumtendea haki kwa sababu hauko huru.

Mahakama inatarajiwa kutoa maumuzi yake katika muda usiozidi siku 90.

Rusesabagina mwenye umri wa miaka 66, alipata umaarufu baada ya mcheza filamu wa Marekani Don Cheadle kumuigiza katika filamu “Hoteli Rwanda”.

Filamu hiyo ilikuwa inaelezea juhudi za Rusesabagina katika kuokoa maisha ya maelfu ya raia kutoka jamii ya wa Tutsi wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994.

.

XS
SM
MD
LG