Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 17:38

Hatma ya dhamana ya Rusesabagina kuamuliwa Alhamisi


Paul Rusesabagina (katikati) alipofikishwa mahakamani akiwa na mawakili wake David Rugaza(kulia) na Emeline Nyembo (kushoto) Mahakama ya Kicukiro, Kigali, Rwanda, Septemba 14, 2020.
Paul Rusesabagina (katikati) alipofikishwa mahakamani akiwa na mawakili wake David Rugaza(kulia) na Emeline Nyembo (kushoto) Mahakama ya Kicukiro, Kigali, Rwanda, Septemba 14, 2020.

Mahakama ya Rwanda inaweza kuamua leo Alhamis, ikiwa mtu ambaye aliigiza katika filamu ya Hotel Rwanda atapewa dhamana baada ya kushtakiwa mapema wiki hii kwa ugaidi.

Serikali ya Rwanda inamhusisha Paul Rusesabagina katika mauaji na kuunda kikundi cha waasi wenye silaha.

Mwanaharakati huyo ambaye ameshikiliwa tangu mwishoni mwa mwezi uliopita, anaomba kuachiliwa kwa sababu ya afya mbaya.

Rusesabagina alikataa kukubali mashtaka yote 13 siku ya Jumatatu, ikiwemo kuhusishwa na mauaji, akidai kuwa mashtaka mengine hayana msingi.

Waendesha mashtaka wanamshutumu Rusesabagina kwa kupanga uhalifu dhidi ya raia wasio na silaha, wasio na hatia wa Rwanda mwaka 2018.

Filamu hiyo ya Hotel Rwanda, ilimuonyesha Rusesabagina aliyekuwa meneja wa Hoteli kama shujaa, ambaye aliwalinda watutsi waliokimbia mauaji ya halaiki mwaka 1994 nchini Rwanda. Anapongezwa kuokoa Maisha ya zaidi ya watu 1,000.

XS
SM
MD
LG