Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 03:29

Watoto wa Rusesabagina wadai baba yao ametekwa nyara na Rwanda


Paul Rusesabagina afikishwa abele ya waandishi habari mjini Kigali Rwanda
Paul Rusesabagina afikishwa abele ya waandishi habari mjini Kigali Rwanda

Familia ya Paul Rusesabagina aliepata umaarufu kutokana na filamu ya Hollywood inayoeelezea namna alivyookoa raia wa ki-Tutsis wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 nchini Rwanda, inawashtumu viongozi wa Rwanda kwa kumteka nyara.

Familia yake imezungumza siku moja baada ya Rusesabagina kuonekana Jumatatu mbele ya waandishi wa habari wa Rwanda akiwa amepigwa pingu. Polisi ya Rwanda imesema Rusesabagina alikamatwa kwa tuhuma za ugaidi chini ya hati ya kimataifa ya kumkamata.

Carine Kanimba, binti wa Rusesabagina ameandika kwenye ukurasa wa facebook yake Jumanne kwamba babake alitekwa nyara na kupelekwa Rwanda kwa kwa njia ya kipekee na ya kisiri ya kuhamisha wahalifu.

Serikali ya Rwanda haijajibu bado tuhuma za familia kwamba Rusesabagina alitekwa nyara.

Rusesabagina alikimbilia uhamishoni baada ya mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda, ambapo alipongezwa na mataifa mengi ya dunia, alipokea tuzo ya juu zaidi ya kiraia ya marekani, kwa kupewa na rais Georges w Bush, medali ya uhuru wa kujieleza hapo mwaka wa 2005.

Lakini baadhi watu walonusurika kutokana na mauaji ya kimbari pamoja na rais wa Rwanda Paul Kagame walipinga maelezo ya Rusesabagina kuwa aliokoa wa Tutsis. Kagame na waathiriwa hao wanamtuhumu Rusesabagina kutumia mauaji ya kimbari kwa maslahi ya biashara. Maafisa wa Ubelgiji wanasema hawana Habari juu ya hali mambo yalivyotendeka na hawakuhusika na kukamatwa kwake.

XS
SM
MD
LG