Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 05:15

Wanaharakati wa haki za binadamu wahoji hukumu dhidi ya Rusesabagina


Baadhi ya washukiwa waliofungwa pamoja na Rusesabagina wakiwa kwenye mahakama Jumatatu

  Makundi ya kutetea haki za binadamu barani Afrika yamelalamikia uamuzi wa mahakama kuu ya Rwanda ya kumfunga jela kwa miaka 25, Paul Rusesabagina ambaye alisifika sana kwenye filamu ya Hollywood ya Hotel Rwanda. 

Mahakama hiyo Jumatatu ilisema kwamba imepata Rusesabagina pamoja na washukiwa wengine 20 na hatia ya ugaidi, madai ambayo alikanusha wakati wakosoaji wa uamuzi huo wakisema kwamba kukamatwa kwake pamoja na kesi dhidi yake havikufikia viwango vya kimataifa vya sheria.

Bahima Macumi ambaye ni raiya wa Rwanda aliyetorokea Kenya zaidi ya miaka 20 iliyopita baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuzuka amesema kwamba amekuwa akifuatilia kwa karibu kesi dhidi ya Sesabagina wakati akisema kwamba uamuzi wa mahakama haukuwa wenye haki.

Katika macho ya ulimwengu kwa ujumla, Rusesabagina ni shujaa ambaye alihatarisha maisha yake kwa kuwapa hifadhi Wahutu na Watutsi kwenye hoteli ya Kigali wakati mauaji yakiendelea mwaka wa 1994 nchini Rwanda.

Lakini machoni mwa serikali ya Rwanda, yeye ni tishio na mkosoaji mkubwa wa Rais Paul Kagame ambaye amedaiwa kuunga mkono kundi la wapiganaji kwa nia ya kupindua serikali wakati huo. Wanaharakati wa haki za binadamu wamekemea hukumu hiyo.

Kulingana na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty Intl’, hukumu ya Jumatatu inatilia mashaka mfumo wa mahakama wa Rwanda ifikapo kwenye kesi za watu mashuhuri au zinazohusiana na masuala nyeti.


Rusesabagina ana hadi siku 30 za kukata rufaa lakini makundi ya kutetea haki za binadamu yana mashaka iwapo mahakama itafanya maamuzi yasiyoegemea upande wowote.

Rusesabagina amesema kwamba alidanganywa kuingia Rwanda Agosti 2020. Aliabiri ndege nchini Dubai akiamini kwamba ilikuwa ikielekea Burundi, lakini badala yake ilitua mjini Kigali Rwanda ambako alikamatwa mara moja.

Februari mwaka huu yeye na wenzake 20 walifunguliwa mashtaka ambayo yalipelekea hukumu ya Jumatatu ya kifungo cha miaka 25 jela. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price pia amehoji uamuzi wa mahakama hiyo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG