Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 00:22

Russia yapiga makombora katika vituo vya nishati Ukraine, huduma muhimu zakosa umeme


Mfanyakazi katika wodi ya wazazi akipeleka chakula kinachotolewa na asasi ya kiraia ya World Central Kitchen, kwa wagonjwa wakati umeme umekatika kufuatia shambulizi la makombora lililofanywa na Russia huko Mykolaiv, Ukraine, Oct. 22, 2022.
Mfanyakazi katika wodi ya wazazi akipeleka chakula kinachotolewa na asasi ya kiraia ya World Central Kitchen, kwa wagonjwa wakati umeme umekatika kufuatia shambulizi la makombora lililofanywa na Russia huko Mykolaiv, Ukraine, Oct. 22, 2022.

Russia imeanzisha upya mashambulizi “mapana zaidi” ya makombora katika vituo vya nishati vinavyosambaza umeme kwa raia kote nchini Ukraine, na kusababisha kukatika umeme nchi nzima, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya kila siku kupitia kanda ya video Jumamosi jioni.

Mamlaka nchini Ukraine zinasema karibu kaya milioni 1.5 kote nchini zimeachwa bila ya umeme.

Lakini Zelenskyy alisema mengi ya makombora na droni za Russia zilikuwa zinatunguliwa, akirejea taarifa ya awali ya jeshi la Ukraine iliyosema kwamba ilitungua makombora 18 kati ya 33 yaliyokuwa yamerushwa kutoka angani na baharini Jumamosi.

Volodymyr Zelenskyy
Volodymyr Zelenskyy

“Bila shaka kwa sasa hatuna uwezo wa kiufundi kutungua asilimia 100 ya makombora na droni za Russia. Nina uhakika, taratibu, tutafanikiwa kufanya hivyo, kupitia msaada kutoka kwa washirika wetu,” Zelenskyy alisema.

Russia imeongeza mashambulizi yake katika vituo vya umeme vya mifumo ya kusambaza maji na miundombinu mingine muhimu nchini Ukraine katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Maeneo yanayoyalenga katika mashambulizi ya karibuni ni pamoja na Khmelnytskiy na Lutsk upande wa magharibi mwa nchi na mji wa katikati wa Uman.

Khmelnytskiy, ambao ni makazi ya watu 275,000 kabla ya vita, hauna umeme, muda mfupi baada ya vyombo vya habari vya ndani kuripoti milipuko kadhaa mikubwa siku ya Jumamosi, maafisa wa mkoa walisema.

Kikosi cha zimamoto kikizima moto uliosababishwa na shambulizi la droni katika majengo kadhaa, Kyiv, Ukraine, Oct. 17, 2022.
Kikosi cha zimamoto kikizima moto uliosababishwa na shambulizi la droni katika majengo kadhaa, Kyiv, Ukraine, Oct. 17, 2022.

Uman, ambao ulikuwa na kiasi cha wakazi 100,000 kabla ya vita, pia umegubikwa na giza baada ya roketi kupiga kituo cha umeme kilicho karibu na mji huo.

Huko Lutsk, mji wenye wakazi 215,000, umeme ulikuwa umeharibiwa upande mmoja baada ya makombora ya Russia kupiga vituo vya umeme vya eneo hilo, kwa mujibu wamaafisa wa eneo hilo.

Mamlaka huko Khmelnytskiy na Lutsk wamewasihi wakazi wake kuweka akiba ya maji “endapo maji yatakatika.”

Mashambulizi ya anga na kukatika kwa umeme pia kumeripotiwa huko Odesa upande wa kusini, mji wa kati wa Dnipro, na Zaporizhzhia upande wa kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Kampuni ya taifa ya nishati, Ukrenerho, imeendelea kuwasihi wananchi wote wa Ukraine kuhifadhi nishati.

Watu wakiwa katika supermarket bila ya umeme, baada ya makombora ya Russia kushambulia eneo hilo la mjini Kyiv, Ukraine, Oct. 22, 2022.
Watu wakiwa katika supermarket bila ya umeme, baada ya makombora ya Russia kushambulia eneo hilo la mjini Kyiv, Ukraine, Oct. 22, 2022.

Katika hotuba yake Jumamosi jioni, Zelenskyy alisema mamlaka zimeweza kurejesha umeme katika mikoa kadhaa ambayo umeme ulikuwa umekatwa ikiwa ni matokeo ya shambulizi hilo.

“Lengo kuu la magaidi hawa ni nishati,” alisema.

Katika mji mkuu, Kyiv, na mikoa inayozunguka hali ya giza ilienea kote siku ya Jumamosi kutokana na mgao wa umeme.

Maafisa wa Ukraine walisema kiasi cha asilimia 40 ya mfumo wa nishati nchini humo umeharibiwa vibaya sana tangu Russia ilipozidisha mashambulizi katika miundo mbinu ya raia nchini Ukraine.

Zelenskyy mapema alieleza kuwa asilimia 30 ya vituo vya umeme vya Ukraine vimeharibiwa na mashambulizi ya Russia tangu Oktoba 10.

Habari hii inatokana na vyanzo vya habari vya mashirika ya habari ya Ukraine RFE/RL Ukrainian Service

XS
SM
MD
LG