Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 14:03

Umoja wa Ulaya watayarisha vikwazo vipya kwa Iran


Bendera ya Umoja wa Ulaya huko Brussels, Belgium, Oktoba 19, 2022. REUTERS
Bendera ya Umoja wa Ulaya huko Brussels, Belgium, Oktoba 19, 2022. REUTERS

Umoja wa Ulaya Jumatano ulitayarisha vikwazo vipya kwa Iran kwa kuipatia Russia  ndege zisizo na rubani wakati Baraza la Usalama la Umoja huo lilipokutana kuhusu mashambulizi ya kiholela ambayo yamesababisha uharibifu nchini Ukraine.

Marekani, Ufaransa na Uingereza ziliomba mjadala wa faragha wa Baraza la Usalama ili kupaza sauti juu ya usafirishaji wa ndege zisizo na rubani, ambazo maafisa wa Magharibi wanasema zinakiuka azimio la Umoja wa Mataifa, ingawa Russia ina mamlaka ya kura ya turufu kuzuia mpango wowote mpya wa vikwazo.

Ukraine kwa wiki kadhaa imeripoti mashambulizi ya Russia ya ndege zisizo na rubani za Iran ziitwazo Shahed-136 ambazo vichwa vyake vililipuka katika mashambulizi ya kujitoa mhanga na imechukua hatua ya kukata uhusiano na Tehran.

Iran na Russia zote zimekanusha matumizi ya ndege hizo zisizo na rubani, huku Tehran ikisema inataka mazungumzo na Ukraine. Lakini Umoja wa Ulaya ulisema Jumatano kuwa umethibitisha kwamba Iran imetoa ndege hizo zisizo na rubani kwa Russia.

XS
SM
MD
LG