Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:45

Russia: Hali ni tete Kherson, Putin tayari kutumia Nyuklia


Raia waotolewa Kherson wakitumia usafiri wa Feri. Russia imesema wanajeshi wa Ukraine wanaingia Kherson kwa nguvu zote. Okt 22, 2022
Raia waotolewa Kherson wakitumia usafiri wa Feri. Russia imesema wanajeshi wa Ukraine wanaingia Kherson kwa nguvu zote. Okt 22, 2022

Maafisa wa Russia walioteuliwa kuongoza sehemu ambazo Russia ilizinyakua kimabavu nchini Ukraine, wamewaambia wakaazi wa sehemu hizo kuondoka mara moja kutokana na kile wamekitaja kama hali tete ya kijeshi huku wanajeshi wa Ukraine wakikaribia kuingia sehemu hizo.

Maelfu ya raia wameanza kuondoka wakivuka mto Dnipro baada ya onyo kwamba Ukraine inajitayarisha kutekeleza mashambulizi makubwa kudhibithi mji wa Kherson.

Watu wamekuwa wakihama Kherson wakiwa wamebeba vitu muhimu kama nguo na chakula.

Wafanyakazi wa wizara ya maswala ya dharura ya Russia wamekuwa wakiwabeba wazee na watoto, wanaoondoka Kherson wanapelekwa Crimea, sehemu ambayo Russia iliinyakua kimabavu kutoka kwa Ukraine mwaka 2014.

Mapigano makali ya kuudhibiti mji wa Kherson, ambao umekuwa chini ya uongozi wa Russia tangu vita vilipoanza Februari 24, yanaonekana kufikia hatua muhimu sana kwa pande zote mbili huku wanajeshi wa Ukraine wakitishia kuwashinda nguvu wanajeshi wa Russia kwenye ukanda wa magharibi wa mto Dnipro.

Kiongozi wa Russia katika eneo hilo amesema kwamba wanapanga kuwaondoa karibu watu 10,000 kutoka Kherson.

Ukraine imeweka amri ya habari kutovuja kutoka Kherson, lakini kamanda wa jeshi la Russia nchini Ukraine Jenerali Sergei Surovikin amesema kwamba hali ya Kherson imekuwa ngumu sana na kwamba Russia inafikiria kufanya maamuzi magumu.

Wizara ya ulinzi ya Russia imesema Jumamosi kwamba wanajeshi wake wamewashinda nguvu wanajeshi wa Ukraine waliojaribu kuingia Kherson.

Rais wa Russia Vladimir Putin amesema kwamba amejitayarisha kutumia silaha za nyuklia iwapo zitahitajika kulinda kile Russia inadai ni ardhi yake.

Hatua ya Russia kunyakua kimabavu sehemu nne za Ukraine, imekosolewa vikali na washirika wa Ukraine na baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

XS
SM
MD
LG