Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 13:19

UN: Muungano wa Russia haujatupa ruhusa ya kuingia maeneo iliyovamia


Denise Brown, (kati) mwakilishi mkazi wa UN na mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Ukraine

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine amesema wakati kipindi cha majira ya baridi  kali kinakaribia, mamilioni ya watu hawana uwezo wa  kufikia misaada ya kibinadamu katika maeneo ambayo hayapo chini ya udhibiti wa serikali na huenda  wanahitajia misaada.

“Ni ukweli kuwa mara kwa mara tunaomba fursa ya kufikia maeneo ya mstari wa mbele katika nchi zote mbili lakini bahati mbaya, Muungano wa Russia haujatupa ruhusa ya kuingia,” Denise Brown, mwakilishi mkazi wa UN na mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Ukraine aliiambia VOA katika mahojiano. “Ni ombi la wazi la kufikisha misaada ya kibinadamu, lenye misingi ya wajibu wa kibinadamu.”

FILE - Matumizi ya nishati mbadala kupika huko mji wa Kivsharivka, Ukraine, Oct. 16, 2022. Wakazi wa eneo hili wamekuwa wakiishi bila ya gesi, umeme na maji kwa kipindi cha wiki tatu.
FILE - Matumizi ya nishati mbadala kupika huko mji wa Kivsharivka, Ukraine, Oct. 16, 2022. Wakazi wa eneo hili wamekuwa wakiishi bila ya gesi, umeme na maji kwa kipindi cha wiki tatu.

Brown alisema wataendelea kuomba ruhusa ya kuingia katika maeneo yanayodhibitiwa na Russia upande wa kusini na mashariki.

Idadi kubwa ya watu wazima nchini Ukraine pia wako katika mazingira hatarishi, na timu zake zinajitahidi kuzifikia jamii zaidi zilizoko katika maeneo ya ndani, vijijini kupitia jumuiya za kieneo.

Kipindi cha Baridi kinawasili

Brown, ambaye aliwasili Ukraine kuchukua wadhifa wake miezi miwili na nusu iliyopita, anahimiza misaada ili kukabiliana na kipindi cha baridi nchi nzima. Timu zake zinaisaidia jamii kukarabati vifaa vya kutoa joto, mapaa yaliyoharibika na kugawa magodoro, mablanketi na nguo zenye joto. Pia wanawasiliana na mahospitali kuwapatia majenereta na vifaa vya kutoa joto vinavyohamishika.

Ukraine ina vipindi vya baridi kali ambayo huanza katikati ya Novemba na kuendelea hadi katikati ya Machi. Viwango vya wastani vya hali ya hewa viko katika hali ya baridi kali sana ambayo hugeuka barafu na theluji nyingi huanguka.

Ikiwa tayari inapitia hali ngumu ya uvamizi wa Russia, mfumo wa joto wa majumbani utakuwa una matatizo zaidi mwaka huu, wakati ndege zisizo na rubani za Russia na mashambulizi ya makombora yakilenga miundo mbinu muhimu katika siku za karibuni.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG