Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 01:18

Russia na Uturuki zimekubaliana kuunda kituo cha kusambaza gesi


Rais wa Russia Vladimir Putin (kulia) na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kushoto) tbaada ya mkutano wao wa Sochi, Russia, Aug. 5, 2022.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema amekubaliana na mwenzake wa Russia Vladimir Putin kuunda kitiuo cha usambazaji gesi nchini Uturuki.

Akiongea na wanachama wa chama chake cha AK katika bunge, Erdogan alisema Putin alisema Ulaya inaweza kupata gesi yake kutokea nchini Uturuki.

Putin wiki iliyopita alipendekeza Uturuki kuwa ni kituo cha usambazji gesi baada ya mabomba ya Nord Stream kwenye bahari ya Baltic kuahribiwa na milipuko mwezi uliopita.

Umoja wa Ulaya, ambayo awali iliigeukia Russia kwa kiasi cha asilimia 40 ya mahitaji yake ya gesi, hata hivyo inatafuta njia nyingine ili kuondoa utegemezi wa gesi kutoka Russia kufuatia uvamizi wa Putin nchini Ukraine mwezi Februari.

Waagizaji wakubwa wa gesi huko EU kama Ujerumani na Italy wamepata njia mbadala na kuweka akiba ya gesi kabla ya majira ya baridi ambayo huenda yakawa ya hali ngumu zaidi kwasababu ya kupanda kwa bei za nishati na khofu ya mgao wa umeme.

Bomba la Nord Stream 2, lilikuwa linaunganisha Russia na Ujerumani, liliharibiwa mwezi uliopita na kiwango kikubwa cha gesi kuvuja.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG