Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:01

Maandamano yanazidi kupamba moto Iran


Maandamano yanazidi kupamba moto Iran huku nchi hiyo ikitunisha misuli yake ya kijeshi nje ya nchi
Maandamano yanazidi kupamba moto Iran huku nchi hiyo ikitunisha misuli yake ya kijeshi nje ya nchi

Tehran imetoa ndege zisizo na rubani kwa Russia ambazo ziliua raia wa Ukraine, kuendesha mazoezi katika eneo la mpakani na Azerbaijan na kulipua maeneo ya Wakurdi nchini Iraq

Wakati maandamano yakipamba moto nyumbani serikali inayoongozwa na viongozi wa kidini ya Iran inatunisha misuli yake ya kijeshi nje ya nchi. Tehran imetoa ndege zisizo na rubani kwa Russia ambazo ziliua raia wa Ukraine, kuendesha mazoezi katika eneo la mpakani na Azerbaijan na kulipua maeneo ya Wakurdi nchini Iraq.

Iran imekanusha kupeleka ndege hizo zisizo na rubani kwa Russia, na Russia imekanusha kuzitumia nchini Ukraine.

Hatua hizo zinaonyesha viongozi wa Iran wakijaribu kukusanya uungwaji mkono wenye msimamo mkali ndani ya nchi hiyo wakati maandamano yakiendelea kuhusiana na kifo cha Mahsa Amini kilichotokea Septemba 16 mwanamke mwenye umri wa miaka 22 aliyefariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi wa maadili nchini humo.

Pia hutumika kama ukumbusho kwa eneo pana la Mashariki ya Kati na Magharibi kwamba serikali ya Iran bado iko tayari kutumia nguvu nje ya nchi na nyumbani ili kuendelea kuwepo madarakani.

XS
SM
MD
LG