Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 04:45

Rais wa mpito wa zamani Liberia afariki akiwa na umri wa miaka 76


Hayati Amos Sawyer
Hayati Amos Sawyer

Aliyekuwa Rais wa muda nchini Liberia Amos Sawyer ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 76.

Amos alikuwa miongoni mwa wanasiasa maarufu sana nchini Liberia na ambaye alikuwa rais wa muda katika miaka ya 1990 wakati wa juhudi za kumaliza vita vilivyoanzishwa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Charles Taylor na ambaye bado anatumikia kifungo gerezani.

Taylor na waasi wake wa NPFL hawakuutambua uongozi wa Sawyer na walimzuia kuondoka katika mji mkuu wa Monrovia wakati wa utawala wake wa mpito uliodumu kwa miaka minne.

Katika kipindi cha baada ya vita vya Liberia, Sawyer, ambaye alikuwa Profesa na mhadhiri wa sayansi ya siasa alihudumu kama mwenyekiti wa tume ya utawala.

XS
SM
MD
LG