Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 08:16

Massaquoi afikishwa mahakamani kujibu mashataka ya vita Liberia


Gibril Massaquoi [Maktaba sept 27 2001]
Gibril Massaquoi [Maktaba sept 27 2001]

Kesi ya kihistoria ya uhalifu wa kivita dhidi ya kiongozi wa waasi anaotuhumiwa kwa kuongoza mapigano wakati wa vita vya Liberia, imeanza kusikilizwa tena hii leo nchini Finland, baada  ya majaji wanaosikiliza kesi hiyo kurejea kutoka Monrovia, walipokuwa wanasikiliza Ushahidi.

Gibril Massaquoi amefika mbele ya mahakama katika mji wa Pirkanmaa na kusikiliza kesi yake kupitia kwa mkalimani wakati upande wa mashtaka uliasilisha kesi ya ubakaji, mauaji na kuwaandikisha Watoto kama wapiganaji wakati wa vita vya pili vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia mwaka 2003.

Massaquoi amekana mashtaka yote dhidi yake na anadai kwamba hakuwepo Liberia wakati makosa yanayodaiwa kufanyika yalitendeka.

Shahidi aliyefichwa na mahakama, alieleza mahakama namna alivyotekwa na mtuhumiwa na kuzuiliwa katika chumba cha mateso nchini Siera Leone kati ya mwaka 2002 na 2003 baada ya Massaquoi kukubali kutoa habari kwa waendesha mashtaka wa mahakama maalum kwa ajili ya Sierra Leone.

Massaquoi, aliyezaliwa mwaka 1970, alikuwa kamanada wa ngazi ya juu katika kundi la waasi la Revolutionary United front – RUF, kundi la Sierra Leone, lililopigana nchini Liberia.

Alihamia Finland mwaka 2008 na kukamatwa mwezi March 2020 baada ya makundi ya kutetea haki za kibinadamu kuchunguza rekodi yake ya vita.

Mahakama ya Finland ilihamia Monrovia kati ya mwezi Februari na April mwaka huu, na kisha mwezi Septemba ili kusikiliza Ushahidi katika kesi hiyo.

Kusikilizwa kwa kesi hiyo kumetajwa kama jambo la kihistoria, kwa sababu watu wachache wamefunguliwa kesi ya uhalifu wa kivita uliofanyika Liberia na hakuna aliyeshitakiwa ndani ya nchi hiyo.

Karibu watu robo milioni waliuawa katika vita hivyo vya kati ya mwaka 1989 na 2003 katika taifa hilo la Afrika magharibi.

XS
SM
MD
LG