Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 06:46

Zaidi ya watu 50 wafariki katika ajali ya mgodi Liberia


Wachimbaji haramu wa migodi kaika kambi ya Dark Forest Liberia

Naibu waziri wa michezo wa Liberia Millias Sheriff, amesema kwamba ajali hiyo ilitokea pale mgodi katika wilaya ya kaskazini magharibi mwa Liberia kuporomoka.

Akizungumza na shirika la habari la AFP katika wilaya ya Grand Cape Mount, anakotoka, waziri Sheriff amesema "karibu watt 50 wanahofiwa wamefariki na timu ya waokozi inawatafuta wachimba migodi ambao huwenda wamekwama ndani ya vifusi vya mgodi huo kufikia Jumanne usiku, lakini hakutoa maelezo zaidi.

Migodi inayochimbwa kiyenyeji ni kawaida kuonekana katika sehemu mbali mbali za Liberia, moja wapo ya matafía maskini duniani yenye utajiri wa dhahabu na alması.

Aidha, naibu msemaji katika afisi ya rais Smith Tobey anasema haifahamiki kulikuwa na watu wangapi katika mgodi huo ajali ilipotokea akisema anasikia kulikuwepo na zail ya yatu 50.

Maafisa wengine wa serikali kutoka wizara husika wamesafiri hadi eneo hilo la ajali lakini hatuna taarifa zaidi zilizotolewa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG