Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 13:44

Watu 29 wafariki katika mkanyagano Liberia


Picha ikinyesha eneo la mji wa Monrovia, Liberia, Oct. 12, 2017.
Picha ikinyesha eneo la mji wa Monrovia, Liberia, Oct. 12, 2017.

Takriban watu 29 waliuawa katika mkanyagano wakati  tukio la kidini katika viunga vya mji mkuu wa Liberia Monrovia, polisi walisema Alhamisi.

Maafa hayo yalitokea usiku wa Jumatano, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Msemaji wa polisi Moses Carter alisema idadi ya waliofariki ni ya muda na huenda ikaongezeka.

Maelezo kuhusu tukio bado hayako wazi. Vyombo vya habari vya ndani vilisema kuwa ni mkusanyiko wa maombi ya Kikristo unaojulikana nchini Liberia kama msalaba uliofanyika katika uwanja wa soka.

Shahidi Emmanuel Gray, mwenye umri wa miaka 26, aliiambia AFP kwamba alisikia kelele kubwa kuelekea mwisho na aliona maiti kadhaa.

XS
SM
MD
LG