Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 19:33

Rais wa Liberia afukuzwa kutoka kwa chama tawala


Rais wa LOiberia, Ellen Johnson Sirleaf.
Rais wa LOiberia, Ellen Johnson Sirleaf.

Chama kinachotawala nchini Liberia, Unity party, kimemfukuza rais anayeondoka wa nchi hiyo, Ellen Johnson Sirleaf, kutoka kwa uanachama

Chama hicho kilipiga kura ya kumwondoa siku ya Jumamposi na hatua hiyo ilichukuliwa baada ya tuhuma kwamba hakumuunga mkono makamu wake wa rais Joseph Boakai kama mgombea urais kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka jana.

Boakai, ambaye alikuwa makamu wa rais kwa miaka 12, alishindwa na nyota wa zamani wa soka, George Waeh.

Johnson Sirleaf, ambaye ni mshindi wa tuzo la amani la Nobel, hangegombea tena urais kwa sababu haruhusiwi na katiba ya Liberia kufanya hivyo.

Wakosoaji wa Boakai walimshutumu kwa kile walichokiita "kutofanya mengi ya kuimarisha taifa" akiwa makamu wa rais.

Iwapo kila kitu kitaenda shwari, Liberia itashuhudia ubadilishanaji mamlaka kwa njia ya kidemokrasia kwa mara ya kwanza katika kipindi cha Zaidi ya miaka 70.

XS
SM
MD
LG