Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 20:00

Raia wa Sudan waandamana tena wakiadhimisha mapinduzi


Raia wa Sudan walipondamana mitaani kupinga utawala wa kijeshi mjini Khartoum Juni 30, 2020. REUTERS/Mohamed Nureldin.
Raia wa Sudan walipondamana mitaani kupinga utawala wa kijeshi mjini Khartoum Juni 30, 2020. REUTERS/Mohamed Nureldin.

Raia wa Sudan wameingia mitaani  kote nchini humo  katika maandamano makubwa ya kupinga unyakuzi wa kijeshi na makubaliano yaliyofuata ambayo yamemrejesha madarakani Waziri Mkuu Abdalla Hamdok lakini yakaweka kando vugu vugu hilo.

Mamlaka ya Sudan iliimarisha usalama katika mji mkuu, Khartoum, na mji pacha wa Omdurman, na kuweka vizuizi katika majengo ya serikali na kijeshi.

Maandamano ya Jumapili yanaadhimisha mwaka wa tatu tangu kuanza kwa uasi ambao hatimaye ulilazimisha kuondolewa na jeshi kwa kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir na serikali yake ya Kiislamu mwezi Aprili mwaka 2019.

Sudan kisha ikafuata njia dhaifu ya demokrasia na kuongozwa na serikali ya pamoja ya kijeshi na kiraia. Mapinduzi ya Oktoba 25 yamepelekea shida katika kipindi cha mpito na kusababisha maandamano yasiyokwisha mitaani.

XS
SM
MD
LG