Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 05:52

Wanajeshi hawatashiriki kwenye uchaguzi ujao Sudan: Burhan


Jenerali Abdel-Fattah al-Burhan mkuu wa taifa na majeshi ya Sudan akizungumza na waandishi habari 26 Oct. 2021.
Jenerali Abdel-Fattah al-Burhan mkuu wa taifa na majeshi ya Sudan akizungumza na waandishi habari 26 Oct. 2021.

Kiongozi wa majeshi wa Sudan Jenerali Fattah al-Burhan akanusha ripoti kwamba wanajeshi na wanamgambo waliyoko kwenye utawala wa mpito wanaweza kugombania viti vya utawala katika uchaguzi wa Julai 2023

Taarifa iliyotolewa na ofisi Burhan siku ya Jumapili inaeleza kwamba “Rais wa Baraza Tawala, anakanusha kile shirika la habari la AFP limeripoti kuhusu kushiriki kwa wanajeshi kwenye uchaguzi mkuu ujao.”

AFP ilimuliza Burhan kwenye mahojiano siku ya Jumamosi, ikiwa wanajeshi na wanamgambo kwenye Baraza la Mpito wataweza kushiriki kwenye uchaguzi ulopangwa 2023.

Burhan alijibu kwa kusema kwamba makubaliano ya Ogusti 2019 yalikua na “kifungu cha wazi kwamba wote wanaoshiriki kwenye kipindi cha mpito hawataruhusiwa kusiriki katika kipindi cha utawala kinachofuata.”

Lakini kwenye makubaliano ya kihistoria ya 2020 na makundi ya waasi, “yalihakikishwa kushiriki kwa baadhi ya wajumbe wa kipindi cha mpito katika serikali inayofuata kipindi hicho”, alisema Burhan.

Katika tarifa iliyotolewa Jumapili inasema Burhan alimaanisha kwamba ni makundi ya zamani ya waasi yaliyotia saini mkataba wa 2020 ndio wanaweza kuwa wagombea kwenye uchaguzi ulopangwa.

Burhan kiongozi wa Sudan tangu kupinduliwa kwa kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir mwezi April 2019 alipindua utawala wa kiraia na kutangaza hali ya dharura Oktoba 25, akifikisha kikomo mpango wa kipindi cha mpito cha miaka mitatu kuelekea utawala kamili wa kiraia.

Lakini Novemba 21, 202, Burhan alitia saini mkataba wa kumrudisha waziri Mkuu Abdalla Hamdok na kumomba aunde serikali mpya.

Mkuu wa Baraza la Mpito la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan, pamoja na waziri mkuu Abdalla Hamdok baada ya kusaini mkataba mpya
Mkuu wa Baraza la Mpito la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan, pamoja na waziri mkuu Abdalla Hamdok baada ya kusaini mkataba mpya

Mahojiano ya Burhan ni moja kati ya mahojiano kadhaa na vyombo vya kimataifa yaliyofanyika siku moja baada ya Katibu Mkuu wau moja wa Mataifa Antonio Guterres, kuanadika kwenye ripoti iliyowasilishwa mberle ya Baraza la Usalama inayoitaja Sudan ina uhasama na waandishi habari.

Ripoti imetokana na Shirika la Habari la Ufaransa AFP

XS
SM
MD
LG