Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 03:48

Polisi wa Sudan watumia gesi ya kutoa machozi kutawanya waandamanaji


Waandamanaji kwenye mji mkuu wa Sudan, Khartoum kwenye picha ya awali

Maafisa wa usalama wa Sudan Jumanne wamelazimika kutumia gesi ya kutoa machozi ili kudhibiti maelfu ya waandamanaji waliojitokeza kwenye barabara za mji mkuu wa Sudan wa Khartoum ikiwa maandamano ya karibuni  ya kupinga mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliopita. 

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, maandamano pia yalishuhudiwa kwenye miji mingine nchini humo. Waziri mkuu aliyekuwa ameondolewa madarakani na jeshi wakati wa mapinduzi hayo Abdalla Hamdock mapema mwezi huu alirejeshwa mamlakani,akiwa chini ya uangalizi wa kijeshi, hatua ambayo wanaharakati wa demokrasia wanaipinga.

Taifa hilo limeshuhudia maandamano makali tangu mapinduzi ya Oktoba 25, yaliopelekea kukamatwa kwa zaidi ya maafisa 100 waliokuwa kwenye serikali ya kiraia. Viongozi wa maandamano hayo mara nyingi wamekuwa wakiomba wanaoshiriki kudumisha amani, lakini mara kwa mara huwa yanamalizikia kwa ghasia.

Vikosi vya usalama vinasemekana kufanya msako mkali dhidi ya waandamanaji wakati tayari watu 43 wakisemekana kufa tangu yalipoanza, kulingana na ripoti ya kamati ya madaktari inyofutilia idadi ya maafa tangu maandamano yalipoanza nchini humo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG