Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 03:06

Maandamano yaendelea Sudan


Maelfu ya waandamanaji wa Sudan walingia katika mitaa ya mji mkuu Khartoum, na sehemu nyingine za nchi Jumatatu, kupinga mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba.

Waandamanaji wamesema polisi walifyatua gesi za kutoa machozi kwa waandamanaji karibu na makazi ya rais.

Shirika la habari la Associated Press, limeripoti kwamba maandamano pia yalifanyika katika miji mingine nje ya mji mkuu Kahartom, Jumatatu, ikijumuisha miji ya Kassala, Sennar, na Port Sudan.

Mapinduzi ya kijeshi yalifanyika Oktoba 25, ambapo dazeni ya maafisa wa serekali ya mpito walikamatwa.

Yalikuwa ni mapinduzi ya pili toka ilipofanyika vuguvugu la Aprili 2019 na kusababisha kuondoka kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir.

XS
SM
MD
LG