Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 23:26

Waziri Mkuu wa Sudan awateua magavana wapya


Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok amewateua magavana wapya katika majimbo ambayo jeshi lilikuwa limejaza nafasi hizo kufuatia mapinduzi ya mwezi Oktoba.

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Hamdok, ambaye alirejea kuwa Waziri mkuu kufuatia makubaliano na jeshi, kufutilia mbali uteuzi uliokuwa umefanywa na jeshi lilipoingia madarakani.

Hamdok vile vile ameteua manaibu mawaziri wapya kuchukua nafasi ya wale waliokuwa wamteuliwa na jeshi kukaimu nafasi hizo.

Baadhi ya waliokuwa wameteuliwa na jeshi katika nafasi hizo ni wale waliokuwa viongozi wakati wa utawala wa Omar al-Bashir aliyepinduliwa kupitia maandamano ya kiraia mwaka 2019.

Hata hivyo, Hamdok hajateua baraza la mawaziri wenye utaalam wa hali ya juu ilivyokubaliwa na jeshi Novemba 21.

Anakabiliwa na changamoto kubwa kuteua baraza lake la mawaziri litakalokubaliwa na vyama vya kisiasa, saw ana waandamanaji.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG