Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:58

Polisi Uganda wasifia tamasha la ‘kwanza’ la Bobi Wine


 Bobi Wine
Bobi Wine

Polisi wamesifia nidhamu na utulivu ulioonyeshwa na mashabiki wa msanii wa muziki wa kizazi kipya na mbunge wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine, aliyefanya tamasha lake la kwanza tangu alipotiwa hatiani kwa mashtaka ya uhaini na kuachiwa.

Lakini katika usiku huo wa Jumamosi polisi waliwakamata washukiwa 80 waliokuwa katika tamasha hilo lililofanyika katika ufukwe wa Busabala, Kampala, Uganda.

Washukiwa hao waliokamatwa na wako rumande kwenye vituo vya polisi vya maeneo ya Kabalagala na Katwe kwa shutuma za kujihusisha na makosa ya wizi wa mfukoni, uvutaji wa dawa za kulevya, kupigana na kuwabughudhi wananchi.

"Ninashukuru polisi wa Uganda kwa kutupa ulinzi na kutotuzuia kama vile walivyokuwa wakifanya siku za nyuma," Bobi Wine aliwaambia mashabiki wake AFP imeripoti.

Bobi Wine amesisitiza kuwa yeye ni mtu anayependa amani na anataka kusikilizwa."

Mbunge huyo mwenye miaka 36 ambaye jina lake ni Robert Kyagulanyi, aliwania kama mgombea huru na kushinda uchaguzi mdogo wa Kyadondo Mashariki.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa idadi ya polisi iliyotumwa kuweka ulinzi tamasha hilo ilikuwa kubwa, na sharti moja la kuruhusiwa kufanyika ni kutojihusisha na siasa.

Bobi Wine ambaye alidai kuwa aliteswa na kupigwa akiwa kuzuizini Agosti 2018, madai ambayo serikali ya Uganda imeyakanusha.

Bobi amejipatia umaarufu mkubwa miongoni mwa vijana nchini Uganda, na wachambuzi wa siasa wanasema kuwa ni mwenye kusababisha taharuki kubwa kwa Rais aliyeko madarakani Yoweri Museveni.

Baadhi ya maelfu ya watu waliohudhuria tamasha walivaa nguo nyekundu, rangi inayohusishwa na vuguvugu la Bobi Wine la People Power (Nguvu ya Wananchi).

XS
SM
MD
LG