Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 02:05

Uganda yakosolewa na Umoja wa Ulaya


Rais Yoweri Museveni
Rais Yoweri Museveni

Umoja wa ulaya umekosoa namna maafisa wa usalama walivyo wakamata wabunge na raia kaskazini mwa Uganda kwa madai kwamba walipiga mawe msafara wa Rais Yoweri Museveni.

Taarifa ya wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya walio jijini Kampala inataka wote walioshiriki katika kuwapiga wabunge na raia katika mazingira yanayotajwa kuwa ni ya kinyama, kuchukuliwa hatua.

Hata hivyo msemaji wa serikali Ofwono Opondo, amekanusha taarifa kwamba wabunge na raia walipigwa, akieleza kwamba maumivu wanayopata wahusika, huenda yanatokana na nguvu zilizotumika wakati walipokuwa wakikamatwa.

Taarifa ya Umoja wa Ulaya inajiri wakati wakili wa Mbunge Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi wine, akiripoti kwamba mbunge huyo, anayezuiliwa katika gereza la kijeshi la Makindye jijini Kampala, hawezi kuongea, kusimama wala kuketi baada ya kupigwa vibaya na kikosi kinachotoa ulinzi kwa Rais Museveni SFC.

Bobi Wine, na wabunge wengine sita, wamefunguliwa mashtaka ya kutaka kupindua serikali ya Rais Museveni kufuatia vurugu zilizozuka, siku ya mwisho ya kampeni katika uchaguzi mdogo wilayani Arua, kaskazini mwa Uganda.

XS
SM
MD
LG