Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 01:27

Palestina : Shambulizi la Israeli Ukingo wa Magharibi laua wapiganaji 4


Watu wakiangalia eneo ambalo Wapalestina watatu waliuawa na shambulizi la jeshi la Israeli huko Beit Anan katika eneo linalokaliwa kimabavu na Israeli Ukingo wa Magharibi, Sept. 26, 2021.REUTERS/Mohamad Torokman
Watu wakiangalia eneo ambalo Wapalestina watatu waliuawa na shambulizi la jeshi la Israeli huko Beit Anan katika eneo linalokaliwa kimabavu na Israeli Ukingo wa Magharibi, Sept. 26, 2021.REUTERS/Mohamad Torokman

Majeshi ya Israeli yamewaua Wapalestina wanne wakati wa mashambulizi huko Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu na Israeli Jumapili, Wizara ya Afya ya Wapalestina imesema.

Waziri Mkuu wa Israeli Naftali Bennett, katika taarifa yake, amesema majeshi ya Israeli yamefanya operesheni hiyo dhidi ya “kikundi cha magaidi cha Hamas ambao walikuwa wamekaribia kufanya mshambulizi.”

Hakusema lolote juu ya vifo vilivyosababishwa na shambulizi hilo nayemsemaji wa jeshi la Israeli hakuwa na maoni ya harakajuu ya mashambulizi hayo.

Maafisa wa Israeli kwa muda mrefu wamekuwa wakieleza wasiwasi wao kwamba Hamas, ambayo inatawala Ukanda wa Gaza, ina azma ya kupata udhibiti wa eneo la Ukingo wa Magharibi na kutoa changamoto kwa mahasimu wao, Mamlaka ya Wapalestina inayoungwa mkono na nchi za Magharibi.

Wizara ya Afya ya Mamlaka ya Palestina imesema Wapalestina watatu waliuawa katika Kijiji cha Biddu huko Ukingo wa Magharibi, kaskazini magharibi mwa Jerusalem. Imesema Mpalestina mwengine aliuawa huko Burqin, kijiji kilichopo karibu na mji wa Palestina, Jenin.

Ripoti za vituo kadhaa vikuu vya radio za Israeli na tovuti za habari zimesema wapiganaji wasiopungua wanne waliuawa katika mashambulizi hayo kwenye maeneo mbalimbali huko Ukingo wa Magharibi yaliyolengwa kuwakamata wanachama wa Hamas.

Chanzo cha Habari Hii ni Shirika la Habari la Reuters

XS
SM
MD
LG