Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 06:18

Israeli yaunda tume kuchunguza matumizi ya programu ya Pegasus


Picha yenye simu inayoonyesha tovuti ya shirika la NSO la Israeli ikiwa na programu ya 'Pegasus' ya udukuzi, kwenye maonyesho Paris on Julai 21, 2021.(Photo by JOEL SAGET / AFP)
Picha yenye simu inayoonyesha tovuti ya shirika la NSO la Israeli ikiwa na programu ya 'Pegasus' ya udukuzi, kwenye maonyesho Paris on Julai 21, 2021.(Photo by JOEL SAGET / AFP)

Israeli imeunda tume ya kukagua madai kwamba programu yenye utata ya ufuatiliaji wa simu ya Pegasus ilitumiwa vibaya, mkuu wa Kamati ya Mambo ya nje ya Bunge amesema Alhamisi.

Taasisi ya ulinzi iliteua tume ya ukaguzi iliyoundwa na vikundi kadhaa, mbunge Ram Ben Barak aliambia Redio ya Jeshi.

Tume itakapomaliza uchunguzi wao, tutadai kuona matokeo na kutathmini ikiwa tunahitaji kufanya masahihisho, naibu mkuu wa zamani wa wakala wa ujasusi wa Israeli Mossad aliongeza.

Pegasus amehusishwa na uwezekano wa ufuatiliaji mkubwa wa waandishi wa habari, watetezi wa haki za binadamu na wakuu wa nchi 14.

Nambari zao za simu zilikuwa miongoni mwa walengwa wa ufuatiliaji 50,000 kwenye orodha iliyopelekwa kwa shirika la haki za binadamu Amnesty International na shirika lenye makao yake Paris Forbidden Stories.

Chanzo cha Habari : VOA News

XS
SM
MD
LG