Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 22:20

Tanzania : Mwili wa hayati Magufuli waagwa rasmi Chato


Mwili wa hayati Rais wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli. Picha na Ofisi ya Rais.
Mwili wa hayati Rais wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli. Picha na Ofisi ya Rais.

Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli umeagwa rasmI leo wilaya ya Chato mkoani Geita mahali alipozaliwa. 

Magufuli alifariki dunia Machi 17 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa ugonjwa wa moyo.

Akizungumza katika shughuli hiyo ya kuuaga mwili wa hayati Magufuli wilayani Chato, Hemed Suleiman Abdulah, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, ambaye ni mwenyekiti mwenza wa kamati ya mazishi kitaifa amewasihi Watanzania kuendelea kushikamana katika kulijenga taifa, ambalo Magufuli ameliacha salama na lenye heshima.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, amesema ni wajibu wa viongozi na Watanzania kuungana kuenzi mazuri yote aliyofanya Hayati Magufuli na kuendeleza sera zake za kuchapa kazi, kupiga vita rushwa na ubadhirifu na kuweka mbele uzalendo na maslahi ya taifa

Dkt Medad Kalemani, Mbunge wa jimbo la Chato kupitia Chama Cha Mapinduzi, CCM, ambaye pia ni Waziri wa Nishati na watu wengine waliofika wilayani Chato na wenyeji wa wilaya hiyo wamezungumzia walivyoguswa na kifo cha rais huyo wa awamu ya tano.

Hayati Magufuli anatarajiwa kuzikwa kesho wilaya ya Chato mkoani Geita katika makaburi ya familia. Atazikwa kwa heshima zote za kijeshi.

XS
SM
MD
LG