Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 18:38

Mvua kubwa yasababisha vifo vya watu 500 DRC


Uharibifu uliosababishwa na mafuriko mjini Goma, DRC.Picha na VOA
Uharibifu uliosababishwa na mafuriko mjini Goma, DRC.Picha na VOA

Zadi ya watu mia tano wamefariki dunia kutokana na mafuriko na kufunikwa na maporomoko ya matope yaliyosababishwa na na mvua kubwa za siku nne mfululizo huko Nyamukubi wilayani Kalehe katika jimbo la Kivu kusini.

Mvua hizo pia zimesababisha uharibifu wa nyumba, ni moja ya maafa makubwa sana katika historia ya hivi karibuni huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Manusura walitazama video zilizochapishwa mitandaoni zikiwaonyesha wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wakirundika maiti kwenye makaburi mapya ya halaiki yaliyochimbwa mwishoni mwa wiki.

Wafanyakazi hao wametumia siku kadhaa kuopoa miili iliyojaa matope kutoka katika vijiji vya Bushushu na Nyamukubi vilivyopo katika mkoa wa Kivu Kusini, ambako mvua kubwa ya siku kadhaa ilisababisha maporomoko ya udongo na mito kuvunja kingo siku ya Alhamisi.

“Tuliacha kila kitu nyuma,” alisema mkazi wa Bushushu, Bahati Kabanga mwenye umri wa miaka 32, ambaye alifanikiwa kumuokoa mtoto wake pekee lakini aliwapoteza shangazi, dada na wapwa zake.

“Tulihisi tetemeko wakati mvua alipokuwa ikinyesha, tukaamua kukimbia baada ya kuona nyumba kwa mbali zikiporomoka," aliliambia shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu.

Serikali kuu mjini Kinshasa bado haijatoa idadi ya vifo. Imetuma wajumbe kwenye eneo hilo na kutangaza Jumatatu siku ya maombolezo ya kitaifa.

Hali ya joto kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa inazidisha kiwango cha mvua za mara kwa mara barani Afrika, kulingana na wataalam wa hali ya hewa wa Umoja Wa Mataifa.

Baadhi ya taarifa ya habari hii, inatoka shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG