Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 11, 2024 Local time: 05:50

Mamia wafariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi DRC

Wanawake wakiomboleza wakikusanyika kutambua maiti katika kijiji cha Nyamukubi, jimbo la Kivu Kusini, nchini Congo Jumamosi, Mei 6, 2023. Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi mashariki mwa Congo.

Idadi ya waliofariki dunia kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi mashariki mwa Congo imeongezeka kupita zaidi ya 400, huku watu wengi zaidi wakiwa bado hawajulikani walipo, kwa mujibu wa vyombo vya habari na mwandishi wa VOA aliyeko mashariki mwa Congo.

Thomas Bakenge, msimamizi wa Kalehe, eneo lililoathiriwa zaidi, aliwaambia waandishi wa habari kwenye eneo la tukio Jumamosi kwamba miili 203 ilikuwa imepatikana hadi sasa, lakini juhudi za kutafuta wengine bado zinaendelea.

Katika kijiji cha Nyamukubi, ambapo mamia ya nyumba zilisombwa na maji, waokoaji na walionusurika walichimba kwenye udongo Jumamosi wakitafuta miili zaidi kwenye matope.

Wanakijiji walilia na kuomboleza walipokusanyika kuzunguka baadhi ya miili iliyopatikana hadi sasa, ambayo ilikuwa kwenye nyasi iliyofunikwa kwa vitambaa vya matope karibu na kituo cha wafanyakazi wa uokoaji.

XS
SM
MD
LG