Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 03:54

Mkurugenzi wa Twitter alaumiwa kwa kudharau mauaji ya Rohingya


Twitter CEO Jack Dorsey testifies before the Senate Intelligence Committee hearing on 'Foreign Influence Operations and Their Use of Social Media Platforms' on Capitol Hill, Sept. 5, 2018, in Washington.
Twitter CEO Jack Dorsey testifies before the Senate Intelligence Committee hearing on 'Foreign Influence Operations and Their Use of Social Media Platforms' on Capitol Hill, Sept. 5, 2018, in Washington.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Twitter amekabiliwa na shutuma kali za kuifagilia Myanmar kuwa ni kituo bora cha utalii pamoja na kuwepo rekodi ya maelfu ya wakimbizi wanaokimbia mateso ya kinyama yanayo endeshwa na jeshi la Myanmar yaliyotajwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni mauaji ya halaiki.

Jack Dorsey aliwatangazia wafuasi wake milioni 4 Jumamosi kwamba alikuwa amezuru Myanmar kaskazini mwezi Novemba kwa siku kumi za kutafakari kwenye eneo lenye utulivu, na kuwashawishi watembelee nchi hiyo.

"Watu wanafuraha tele na chakula ni cha kipekee," aliwashauri wafuasi wake kutembelea huko.

Lakini hilo limeibua lawama kutoka kwa baadhi watu wakisema amepuuza hatma ya walio wachache katika jamii ya Kiislam ya Rohingya wanaoishi Myanmar.

Jeshi la Myanmar, mwaka 2017, liliripotiwa kuanzisha operesheni ya kuwasaka wanamgambo wa Rohingya baada ya vituo kadhaa vya polisi kushambuliwa.

Maelfu ya watu wameuawa na taasisi zinazopigania haki za binadamu zinasema jeshi lilichoma nyumba na ardhi na kuendesha mauaji na ubakaji.

Wakati majeshi ya Myanmar yakifanya mashambulizi hayo dhidi ya wanamgambo wa Rohingya, yanayo daiwa na vikundi vya haki za binadamu kupitiliza mipaka, na watu zaidi ya 700,000 wa jamii ya Rohingya walikimbilia nchi jirani ya Bangladesh kutafuta hifadhi, baada ya makazi yao na ardhi zoa kuharibiwa kwa kuchomwa moto.

Umoja wa Mataifa umetaja kitendo hicho cha jeshi la Myanmar kuwa ni mfano wa kuiangamiza jamii na kusema kuwa maafisa wa vyeo vya juu nchini Myanmar wanastahili kuchunguzwa kwa makosa ya jinai ya uhalifu wa kivita.

XS
SM
MD
LG